July 14, 2015

MANJI
saa chache badaa ya jeshi la polisi tanzania kutoa ufafanuzi kuhusiana na fedha zilizoelezwa kuwa ni mali ya kampuni ya quality group inayomilikiwa na mwenyekiti wa yanga, Yusuf manji. yeye ameamua kutoa ufafanuzi zaidi, soma.


TAARIFA KWA UMMA

1.   Siku ya Jumapili tarehe 12 Juli, 2015, kulikuwa na habari nyingi za uongo na zenye madai ya kashfa na maneno ya uchochezi ambayo yalichapishwa katika vyombo vya habari vyenye sifa mbaya kwa jamii vya Reginald Mengi vilivyo chini ya makampuni ya IPP ambavyo vilikuwa na vichwa vya habari vya ajabu kama vilivyotoka katika magazeti ya:

a.   Guardian On Sunday ambapo kulikuwa na kichwa cha habari cha “Wakala wa Manji akamatwa katika njama za kutoa rushwa ya Sh 700m”;

b.   NipasheJumapili ambalo lilichapisha kichwa cha habari cha  “Millioni 700/- za Manji zanaswa hotelini Dodoma”; na

c.   Televisheni ya ITV  iliyotangaza katika Taarifa ya Habari ya Jumamosi, Julai 11, 2015 na Jumapili, Julai 12, 2015 ikirudia habari za magazeti yaliyotajwa hapo juu.

Habari hizi za ajabu zilizotolewa na vyombo hivyo vya IPP zilianzisha uvumi huo katika mitandao ya jamii ikiwa ni pamoja na kusambaza picha pamoja na simulizi za uongo wa kuchekesha..

2.   Ukweli halisi ni kwamba tarehe 10 Julai, 2015, Bw.  Amit Kevalramani aliwasili kwa ndege binafsi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ili kupeleka fedha za kununua mchele na mahindi mkoani  wa Dodoma katika kampuni la M/s Tanrice Grains & Pulses Limited –  kampuni tanzu la  M/s Quality Group Limited, ambalo Mwenyekiti wake ni Bw.  Yusuf Manji.

3.   Bw. Amit Kevalramani alikuwa akutane tarehe hiyo ya Julai 10, 2015 na watu wenye kuhusika na manunuzi kutoka kampuni ya M/s Tanrice Grains & Pulses Limited, ambapo Bw.  Amit Kevalramani alikuwa amepanga kurejea kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa ndege ya saa 3:30 siku ya Jumamosi, Julai 11, 2015.

Mkutano huo ulichelewa, na Bw.  Amit Kevalramani alipewa tiketi nyingine ya ndege kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ambayo ingeondoka saa 10:30 siku ya Jumamosi, Julai 12, 2015.

4.   Kunako kama saa 3:30 asubuhi, Bw. Amit Kevalramani aliondoka katika hoteli yake, na wakati akielekea kwenye gari alilokuwa amekodishiwa, alivamiwa na wezi na katika mapambano yaliyotokea, begi moja lililokuwa na fedha lilichanika, na hivyo kuwafanya maofisa usalama kufika mara moja katika eneo hilo.


Baada ya kuona njama zao zimekwama, wezi hao wakajifanya kuwa wafuasi wa CCM waliokuwa wamepanga katika hoteli hiyo na kuanza kupiga makelele wakisema “rushwa”, jambo ambalo liliwavuta watu wa vyombo vya habari kwenda hapo.

5.   Katika mkanganyiko huo, Jeshi la Polisi la Dodoma lilikuwa makini katika kufanya kazi yake ambapo lilizikusanya fedha zote na Bw. Amit Kevalramani akahakikisha fedha zake zote zipo na zilikuwa salama.  Pia,  kutokana na maombi yetu, jeshi la polisi lilihakikisha Bw. Amit Kevalramani anawekwa mahali penye usalama ambapo asingefikwa na tishio lolote  la kuibiwa fedha hizo.  Tulifanya hivyo tukijua kwamba kutokana na habari potofu zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya IPP vya Reginald Mengi, Bw. Amit Kevalramani (pamoja na fedha ambayo alikuwa amekabidhiwa) vilikuwa tayari ni lengo la makundi ya majambazi na makundi ya kisiasa yaliyokuwa yamekata tamaa.

6.   Jioni ya Jumamosi, Julai 11, 2015, Bw.  Amit Kevalramani alichukuliwa na maofisa  wa kampuni letu la usalama na siku ya Jumapili, Julai 12, 2015, akiwa na fedha zote kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi la Dodoma ambalo lilithibitisha kwamba fedha hiyo aliyokuwa nayo Bw. Amit Kevalramani ilikuwa ni halali, na hivyo Bw.  Amit Kevalramani akiwa na fedha hiyo, akasafiri kwa ndege na kurejea Dar es Salaam salama.

7.   Kampuni la M/s Tanrice Grains & Pulses Limited & Quality Group Limited, linatoa shukurani kwa Jeshi la Polisi Tanzania kwa utatuzi wa haraka wa suala hilo, na linampongeza Bw.  Amit Kevalramani kwa ushupavu wake wa kukabili jaribio hilo la wizi.

8.   Tunachukua fursa hii kuwakumbusha Watanzania kwamba  Reginald Mengi na Yusuf Manji wana mgogoro kati yao ambao umechukua miaka ipatayo kumi.  Majuzi ulipotolewa mwaliko na Yusuf Manji kwa Reginald Mengi wafanye mdahalo wa moja kwa moja Julai 3, 2015, ili “kuufichua ukweli” kuhusu jambo hili, Reginald Mengi alikataa. (Kwa maelezo zaidi ingia  www.manjivsmengi.com)

9.   Habari zilizochapishwa na vyombo vya habari vya IPP  kuhusu suala hili ni mfano mwingine wa jinsi Reginald Mengi alivyozama katika imani ya kusema vitu visivyo sahihi siku zote akitumia vyombo vyake vya habari na kutaka kujaribu kumwonyesha Bw. Yusuf Maji katika mwanga hasi.  Badala ya kufanya hivyo, jamii nayo ni lazima ivilazimishe vyombo vya IPP kujibu maswali muhimu ya kawaida kabla ya kuyachapisha, kama vile:

A.  Ni kwa nini katika machapisho na taarifa zote kuhusu suala hili, hakuna hata mtu mmoja kutoka katika Jeshi la Polisi la Dodoma alihojiwa ili kuthibitisha habari zilizoandikwa na vyombo vya habari vya Reginald Mengi?

B.  Je, kampuni la Quality Group of Companies lenye wafanyakazi wapatao 5,000 humfanya Mengi kuwa na fikra za ajabu kwamba kila mfanyakazi wa kampuni hilo ni “wakala” wa Bw. Yusuf Manji, au kwamba kulitaja jina la Mwenyekiti wa klabu ya Yanga huongeza mapato ya vyombo vyake vya habari?

C. Kwa nini, katika matukio ya rushwa ambayo huhusisha pande mbili, yaani mtoaji na mpokeaji, vyombo vya habari vya IPP vilimtaja “mtoaji” tu na si mpokeaji?

D. Kwa nini wakati CCM inaendesha shughuli zake, Reginald Mengi alitaka ulimwengu usimame na kufuatilia mambo yake ya kizamani aliyokuwa ameyabuni katika vyombo vyake vya habari dhidi ya kampuni ya Quality Group ambayo  inashiriki kwa kiwango kikubwa kuimarisha uchumi wa nchi hii? 

E.  Kwa nini na kwa namna gani kiasi kidogo cha fedha cha Sh. Milioni  722.5 (sawa na Dola za Marekani 321,000) kiweze kubadili taswira za kisiasa nchini, kutokana na madai yanayotoka kwa mmiliki wa vyombo vya habari ambaye hudai kipato chake cha jumla ni zaidi ya Sh. Trilioni 1.24 trillion au Dola za Marekani milioni 550?

F.  Kwa nini mtu ambaye amekabidhiwa na kampuni la Quality Group kiasi cha fedha ambacho ni sawa na Dola za Marekani 321,000 tu, achukuliwe kwamba alikuwa anatenda kosa la jinai kuwa na fedha hizo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Mengi, wakati gharama ya kuihudumia klabu ya Yanga kila msimu wa ligi katika misimu mitano iliyopita kiasi hicho cha fedha ni kidogo mno kikilinganishwa na kile kinachotolewa na Quality Group?

10.                Kuhusiana na mdahalo wa moja kwa moja wa televisheni uliokuwa umepangwa kufanyika Julai 3, 2015, kati ya Bw. Yusuf Manji, Mwenyekiti wa Quality Group Limited  na  Young Africans Sports Club ambapo  Reginald Mengi aliogopa kuhudhuria,  Bw.  Yusuf Manji bado anatoa mwaliko mwingine kwa Reginald Mengi kuja na ushahidi kwamba  Bw. Yusuf Manji ni mtoa rushwa, na ayaseme yote hayo katika madahalo huo ili kuwaacha Watanzania waamua wenyewe kuhususuala hili.

.
Tunaamini  kwa dhati kwamba kutokana na mwaliko huu wa Bw. Yusuf Manji, Bw. Mengi atajitoleza na asitake kujificha kwenye vyombo vyake vya habari anavyovimiliki bali ajitokeze na kuwapa fursa Watanzania kuamua kilicho kweli badala ya kueneza vitu visivyo sahihi hata kidogo.




(QUALITY GROUP LIMITED)

1 COMMENTS:

  1. Kuna walakini, taarifa ya polisi haijaeleza suala la wezi, mbona kama Kuna kupingana kati ya taarifa mbili, hao wezi waliojifanya wanaccm hawakugunduliwa na polisi, na kama wao ndio walioijuza polisi kwanini wasikamatwe. Ipo siku kitaeleweka.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic